Ruka hadi maudhui

Hali ya majaribio: rekodi zenye alama ya "Mfano" ni za kujaribu muundo tu, si taarifa rasmi.

TANCCOOPSLTD Cotton Co-operatives Joint Enterprise

Kuhusu TANCCOOPS

Maadili Yetu ya Msingi

Misingi saba inayoongoza jinsi tunavyowatumikia wanachama na wadau.

01

Kufanya kazi kama timu

Mafanikio yatahakikishwa kwa kuwepo ushirikiano wa karibu ambao utaongeza ubora wa huduma kwa wanachama.

02

Uwajibikaji

TANCCOOPS LTD inawajibika kwa wanachama wake, serikali na wadau wengine, na itahakikisha utamaduni wa uwajibikaji unazingatiwa na wadau wote wa ndani na nje, kila mmoja na kwa pamoja.

03

Mtazamo kwa wateja

Katika bidhaa na huduma zote zinazotolewa, TANCCOOPS LTD itahakikisha kuwa inazingatia mahitaji halisi ya wakulima.

04

Uwazi

TANCCOOPS LTD ina wajibu wa kuhakikisha uwazi unakuwepo wakati wote inapowasiliana na wadau wake, huku mawasiliano ya ndani na mashirikiano yakiimarishwa hadi kiwango cha juu.

05

Utaalamu

Katika shughuli zote, TANCCOOPS LTD itazingatia maadili ya kitaaluma na viwango vya juu ili kutoa huduma bora na kwa ufanisi kwa wanachama wote.

06

Uaminifu

TANCCOOPS LTD itaendeleza kiwango cha juu cha uaminifu katika kuwatumikia wanachama wake na wadau wengine.

07

Kujitolea

Wajumbe wa Bodi na wafanyakazi wanatarajiwa kufanya kazi wakati wote kwa kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wanachama na wadau wengine.

Misingi ya ushirika

Maadili yetu ya msingi yanatokana na misingi ya ushirika. Ili kufikia maadili haya, misingi ifuatayo itazingatiwa.

  • Uwazi na demokrasia katika umiliki
  • Ushiriki wa kiuchumi
  • Uhuru wa umiliki na usimamizi
  • Elimu, mafunzo na usambazaji wa habari
  • Ushirikiano kati ya wanaushirika na jamii

Chanzo: nyaraka rasmi za TANCCOOPS LTD.

Tushirikiane kuendeleza sekta ya pamba

Iwe wewe ni chama mwanachama, mdau wa serikali, mwekezaji au mbia wa maendeleo โ€” tuko tayari kushirikiana nawe.