Ruka hadi maudhui

Hali ya majaribio: rekodi zenye alama ya "Mfano" ni za kujaribu muundo tu, si taarifa rasmi.

TANCCOOPSLTD Cotton Co-operatives Joint Enterprise

Kuhusu TANCCOOPS

Utangulizi

Historia, usajili na wajibu wa TANCCOOPS LTD.

TANCCOOPS LTD

Tanzania Cotton Co-operatives Joint Enterprise Limited

Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya Pamba Tanzania

Tanzania Cotton Cooperative Joint Enterprise (TANCCOOPS LTD) ni mradi wa pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyojishughulisha na zao la pamba nchini Tanzania.

TANCCOOPS LTD ilianzishwa na kusajiliwa rasmi kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013, tarehe 26 Februari 2020, ikiwa na Namba ya Usajili AFF-SHY-SHY-MC-2023-100. Makao makuu ya TANCCOOPS LTD yapo mkoani Shinyanga, huku wanachama wake wakiwa katika mikoa minane (8) ya Tanzania Bara.

Hadi sasa, TANCCOOPS LTD ina wanachama 13, ambao wote ni Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyohusika na zao la pamba nchini Tanzania.

Lengo kuu la kuanzishwa
β€œKuimarisha maendeleo ya wakulima wa pamba kupitia mfumo wa Ushirika wenye nguvu, uwazi na tija katika upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji, uuzaji na usimamizi wa zao la pamba nchini.”

Wanachama kwa mkoa