Ruka hadi maudhui

Hali ya majaribio: rekodi zenye alama ya "Mfano" ni za kujaribu muundo tu, si taarifa rasmi.

TANCCOOPSLTD Cotton Co-operatives Joint Enterprise

Kuhusu TANCCOOPS

Madhumuni na Malengo

Madhumuni rasmi, malengo ya miaka mitano na vyanzo vya mapato vya TANCCOOPS LTD.

Madhumuni ya Mradi

Madhumuni Yetu

Madhumuni ya TANCCOOPS LTD kama yalivyoainishwa (a)โ€“(k).

Madhumuni ya Mradi ni kukuza na kustawisha matakwa na hali ya kiuchumi ya wanachama kwa kupanga, kusimamia na kuboresha shughuli za maendeleo ya kilimo cha pamba na wanachama wao kwa kuzingatia misingi na matakwa ya ushirika.

(a)

Maendeleo ya kiuchumi kiushirika

Kuandaa, kusimamia, kuratibu, kupanga, kuhamasisha na kukuza maendeleo ya kiuchumi kiushirika miongoni mwa wanachama wake.

(b)

Kupokea, kuchakata na kuuza pamba

Kupokea, kuhifadhi, kuchakata na kuuza bidhaa za zao la pamba mbegu.

(c)

Pembejeo na zana za kilimo

Kununua, kuhifadhi, kuchakata na kusambaza pembejeo na zana za kilimo kwa wahitaji, vikiwemo vyama vya ushirika na wanachama wake.

(d)

Majengo, mitambo na viwanda

Kujipatia, kuendesha, kupangisha, kukodisha majengo na mitambo na viwanda na kumiliki ardhi.

(e)

Uchukuzi na usafirishaji

Kumiliki magari kwa ajili ya shughuli za uchukuzi na usafirishaji wa mazao, zana na pembejeo za kilimo.

(f)

Uwekezaji

Kununua hisa na kuwekeza katika taasisi za umma, taasisi binafsi na vyombo vingine vya kiuchumi kwa idhini ya Mkutano Mkuu na ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika.

(g)

Mikopo na misaada ya kifedha

Kutoa mikopo na misaada ya kifedha kwa wanachama wake kwa kuzingatia sheria na kanuni za Ushirika, masharti ya Mradi pamoja na miongozo ya kisheria inayoweza kutolewa mara kwa mara.

(h)

Mashamba ya mfano na mbegu bora

Kuendesha vituo vya majaribio ya kilimo na mashamba ya mfano na uzalishaji wa pamba na mbegu bora kwa manufaa ya vyama vya ushirika na wanachama wake pamoja na sekta ya kilimo cha pamba kwa ujumla.

(i)

Jukwaa la wadau

Kuwa jukwaa la majadiliano, mashauriano, na maridhiano kati ya vyama vya ushirika vya pamba na wadau wengine wa tasnia ya pamba kwa ujumla.

(j)

Uwakilishi wa vyama vya pamba

Kuwakilisha vyama vya ushirika vya pamba katika majukwaa (Fora) kuhusiana na tasnia na biashara ya pamba kwa ujumla.

(k)

Kiungo na Serikali na wadau

Kuwa kiungo kati ya vyama vya ushirika vya pamba na wanachama wake, serikali na wadau mbalimbali kuhusu tasnia ya pamba katika kukuza, kuendeleza na kuboresha uchumi wa wanachama na wa taifa kwa ujumla.

Malengo ya TANCCOOPS LTD kwa miaka 5

Mwelekeo Wetu wa Kimkakati

Malengo yanayopimika yaliyowekwa na TANCCOOPS LTD, kama yalivyoainishwa katika nyaraka rasmi.

Malengo ya kiutendaji

  1. 1 Kuwezesha shughuli za vyama wanachama
  2. 2 Kutoa huduma kwa vyama wanachama kama itakavyoainishwa kwenye masharti ya vyama vya upili
  3. 3 Kukusanya, kusindika na kuuza bidhaa za vyama wanachama
  4. 4 Kutoa huduma za ushauri elekezi kwa vyama wanachama
  5. 5 Kutoa taarifa zinazohusiana na shughuli zake
  6. 6 Kufanya jambo lingine lolote linalohusiana au litakalosaidia utekelezaji wa madhumuni yaliyoainishwa

Malengo yanayopimika

Lengo 7 Ifikapo 2028

200 1,000

kg / ekari

Kuongeza tija ya uzalishaji

Kuongeza tija ya uzalishaji wa pamba kutoka wastani wa kilo 200 hadi kilo 1,000 kwa ekari moja, na mazao ya pamba, dengu, choroko, alizeti na mpunga kwa 250% ifikapo 2028.

Lengo 8 Ifikapo 2028

+20%

Kupanua eneo la uzalishaji

Kuongeza eneo la uzalishaji wa mazao kwa 20% ifikapo 2028.

Lengo 9 Ifikapo 2028

90%

Pamba daraja la kwanza

Kuboresha ubora wa mazao

Kufikia 90% ya zao la pamba daraja la kwanza na kuongeza ubora kwa 85% kwa zao la mpunga na alizeti ifikapo 2028.

Lengo 10 Ifikapo 2023

50%

Soko la mazao ya kimkakati

Kuongeza sehemu ya soko

Kuongeza idadi na kiwango cha bidhaa katika soko ili kumiliki soko la mazao ya kimkakati kwa 50% ifikapo 2023.

Lengo 11 Ifikapo 2028

1 12

watendaji

Kuimarisha uwezo wa kitaasisi

Kuimarisha ufanisi wa utendaji katika chama kwa kuongeza watendaji kutoka 1 hadi 12 ifikapo 2028.

Lengo 12 Ifikapo 2028

Kuongeza vyanzo vya mapato

Kuongeza vyanzo vya mapato ya Mradi ifikapo 2028.

Takwimu na tarehe zimehifadhiwa kama zilivyo katika nyaraka rasmi.

Vyanzo vya mapato ya TANCCOOPS LTD vitatokana na:

Vyanzo vya Mapato

Biashara na shughuli zinazoiwezesha TANCCOOPS LTD kujiendesha kwa uendelevu.

(a)

Ushuru wa usindikaji mazao

(b)

Hisa za uanachama

(c)

Ziada halisi ya shughuli za Mradi

Kama vile ushuru wa usindikaji, mauzo ya pembejeo na kamisheni katika usambazaji wa vifungashio.

(d)

Mikopo

Kutoka benki, asasi nyingine za fedha na mifuko ya hifadhi ya jamii.

(e)

Misaada na ruzuku

Kutoka taasisi na asasi nyingine.

(f)

Michango ya vyama wanachama

Kwa ajili ya kufanyiwa biashara kama ilivyo katika masharti ya Chama.

(g)

Mapato mengine halali

Viingilio, ada, mauzo ya masharti, vitabu, vitambulisho, fomu mbalimbali na michango maalum kutoka kwa wanachama.

Chanzo: nyaraka rasmi za TANCCOOPS LTD.